Kenya, Haiti zasaini makubaliano ya kutuma polisi
1 Machi 2024Rais William Ruto wa Kenya aliyasema hayo siku ya Ijumaa (Machi 1) baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry, aliyewasili katika taifa hilo la Afrika Mashariki siku ya Alhamis.
Kulingana na Ruto, yeye na mgeni wake walijadiliana hatua zitakazofuata kuharakisha mchakato wa kupeleka polisi 1,000 wa Kenya nchini Haiti.
Soma zaidi: Maafisa wanne wa polisi wauawa Port-au-Prince
Lakini haikubainika wazi ikiwa makubaliano yaliyofikiwa yangelitimiza matakwa ya uamuzi wa mahakama uliotolewa mwezi Januari, ambao ulisema hatua ya kupeleka polisi wa Kenya kisiwani Haiti ni "kitendo kinachokinzana na sheria."
Kwenye nchini Haiti, polisi wanne waliuawa siku ya Ijumaa, huku mmoja wa viongozi maarufu wa magenge akitishia kumtimua madarakani Waziri Mkuu Henry.