1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya Airways yapata hasara nyengine

28 Machi 2023

Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways, limesema limepata hasara ya dola milioni 290 katika kipindi cha mwaka uliopita, kiwango cha hasara ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika historia ya shirika hilo.

https://p.dw.com/p/4PMq5
Kenya Airways Boeing 737-800, vermisstes Flugzeug
Picha: AP

Mwenyekiti mtendaji wa wa shirika hilo, Michael Joseph, akitangaza hali ya shirika hilo amesema hasara iliyorekodiwa kabla ya kodi ni shilingi bilioni 38.3 za Kenya ambazo ni sawa na dola milioni 290 ikilinganishwa na hasara iliyowahi kushuhudiwa mwaka juzi ya shilingi bilioni 16. 

Kwa maana hiyo, shirika hilo la ndege la Kenya linalokabiliwa na matatizo limeshuhudia ongezeko la hasara zaidi ya mara mbili.

Soma zaidi: Kenya Airways kuruka moja kwa moja hadi Marekani

Kwa miaka kadhaa sasa, shirika hilo linalotamba kwa kauli mbiu yake ya ''Fahari ya Afrika'' limekuwa likijiendesha kwa hasara licha ya serikali kumwaga  mamilioni ya dola kulipiga jeki.

Mara ya mwisho Kenya Aiways kupata faida ni mwaka 2012.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW