1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMyanmar

Watu 30 wanaolipinga Jeshi Myanmar wauawa katika shambulizi

11 Aprili 2023

Karibu watu 30 wameuawa nchini Myanmar, baada ya jeshi kuwashambulia watu waliohudhuria tukio lililoandaliwa na wapinzani wa utawala wa kijeshi nchini humo.

https://p.dw.com/p/4Pu3k
 Myanmar | Demo für die Unterstützung National League for Democracy (NLD) Partei
Picha: Hkun Lat/Getty Images

Baadhi ya vyombo vya habari katika eneo kulikotokea shambulizi hilo la Sagaing vimeripoti idadi ya waliofariki imefikia 50, ikiwa ni pamoja na raia.

Shirika la habari Reuters, hata hivyo, halikuweza kuthibitisha taarifa hizi na msemaji wa jeshi hakupatikana kwa simu kuzungumzia hilo.

Utawala wa kijeshi nchini Myanmar  ulioipindua serikali mwaka 2021 umekuwa ukikosolewa na jamii ya kimataifa kutokana na hatua kali dhidi ya wapinzani wake pamoja na raia.