1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMyanmar

Myanmar yakifuta chama cha Suu Kyi

Hawa Bihoga
29 Machi 2023

Tume ya uchaguzi ya Myanmar iliojaa viongozi wa kijeshi imetangaza kukifuta chama cha National League for Democracy NLD cha Aung San Suu Kyi.

https://p.dw.com/p/4PQC0
Myanmar | Militärparade in Naypyitaw | Min Aung Hlaing
Picha: Aung Shine Oo/AP Photo/picture alliance

Tume hiyo ya uchaguzi ya Myanmar imekiuta chama hicho cha National League for Democracy NLD cha Aung San Suu kwa kushindwa kukihuisha chini ya sheria mpya ya uchaguzi. Siku ya Jumatatu mkuu wa utawala wa kijeshi Min Aung Hlaing aliapa mbele ya maelfu ya wanajeshi kwamba hatakata tamaa katika kushughulikia upinzani na kuwahakikishia juu ya kufanyika kwa uchaguzi ingawaje hakutoa ratiba. Mapema mwezi Januari utawala huo wa kijeshi ulitoa muda wa miezi miwili kwa vyama vya siasa kujiandikisha upya chini ya sheria kali ya uchaguzi kabla ya uchaguzi ambao wapinzani wanasema hautakuwa huru na haki. Kati ya vyama 90 vilivyokuwepo ni vyama 50 pekee vilivyotuma maombi ya kujiandikisha upya. Suu Kyi alianzisha NLD mwaka wa 1988 na akashinda ushindi wa kishindo katika chaguzi za 1990 ambazo zilibatilishwa na serikali ya wakati huo.