1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

Kansela wa Ujerumani kuzuru Kenya na Ethiopia

2 Mei 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz atazitembelea Ethiopia na Kenya baadaye wiki hii kwa ziara itakayogusia masuala ya Haki za Binadamu na kutafuta ushirkiano kwenye sekta ya nishati.

https://p.dw.com/p/4Qo2j
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anatarajiwa kuzungumzia ukiukwaji wa haki wakati wa vita katika jimbo la Tigray.
Mzozo katika jimbo la tigray ulisabbaisha mzozo mkubwa wa kibinaadamu na wengi kuyakimbia makazi yao.Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Kansela Olaf Scholz atawasili Ethiopia siku ya Alhamisi ambapo amepangiwa kuwa na mkutano na waziri mkuu Abiy Ahmed mjini Addis Ababa.

Kiongozi huyo ataliweka mezani suala la ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Ethiopia tangu taifa hilo lilipotumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya serikali kuu na jimbo la Tigray mwaka 2020.

Baadaye Scholz atayatembelea makao makuu ya Umoja wa Afrika kabla ya kuelekea nchini Kenya. Serikali ya Ujerumani inaizingatia Kenya kuwa mshirika muhimu kwenye sekta ya nishati rafiki kwa mazingira.

Kansela Scholz atajadili njia za kukuza ushirikiano kwenye eneo hilo hususani uwezekano wa Ujerumani kuanza kuiuzia Kenya nishati ya Haidrojeni.