UchumiDenmark
Kampuni ya meli ya Maersk kuikwepa njia ya Bahari ya Sham
5 Januari 2024Matangazo
Kampuni hiyo ya Denmark imechukua hatua hiyo ikitoa sababu za kiusalama.
Mnamo siku ya Jumanne, Maersk iliweka wazi kuwa haitotumia tena bahari ya Sham na mfereji wa Suez "mpaka hali itakapobadilika" baada ya meli ya Maersk Hangzhou iliyokuwa inatokea Singapore kushambuliwa.
Tangu Novemba 18 mwaka uliopita, meli 25 za kibiashara zinazofanya safari zake kusini mwa Bahari ya Sham na Ghuba ya Aden zimeshambuliwa.
Bahari ya Sham na mrereji wa Suez ni moja kati ya njia muhimu za biashara ya kusafirisha mafuta duniani.
Hii ni mara ya pili kwa kampuni ya Maersk kusitisha safari zake katika bahari ya Sham.