SiasaAsia
Maersk yaendeleza kuzuia usafirishaji kwa njia ya bahari
3 Januari 2024Matangazo
Katika taarifa yake kampuni hiyo imesema endapo itaweza kueleweka na wateja wao meli zao zitabadili uelekeo wa kupita na kuendelea na safari kuzunguka kwa kupitia eneo la bahari la Rasi ya Tumaini Jema. Jumapili iliyopita meli ya Maersk Hangzhou, yenye kupeperusha bendera ya Singapore, inayomilikiwa na Denmark iliyokuwa ikitoka Singapore kuelekea Port Suez nchini Misri, iliripoti kupigwa na kombora wakati ikivuka ujia wa bahari wa Bab al-Mandab.Hii ni mara ya pili kwa Maersk kusimamisha usafirishaji kupitia ujia huo wa bahari. Katikati ya mwezi wa Desemba, kama ilivyo kwa makampuni mengine makubwa ya kimataifa ya meli, kampuni ya Denmark ilisitisha kupitia meli zake kupitia ujia huo, kufuatia mashambulizi ya waasi wa Huthi nchini Yemen.