1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Kamala na Walz kuyatembelea majimbo muhimu kwa uchaguzi ujao

7 Agosti 2024

Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic, Kamala Harris na mgombea mwenzake, gavana wa jimbo la Minnesota, Tim Walz kuyatembelea majimbo yenye ushindani.

https://p.dw.com/p/4jCQb
Kamala Harris na mgombea mwenzake, gavana wa jimbo la Minnesota, Tim Walz
Kamala Harris na mgombea mwenzake, gavana wa jimbo la Minnesota, Tim Walz.Picha: Matt Rourke/AP/dpa/picture alliance

Wanalenga kuitumia siku yote ya leo ili kuwaleta pamoja watu wa chama hicho kwenye majimbo ya kati ya Magharibi mwa Marekani yanayozingatiwa kuwa yamegawika.

Majimbo hayo ni miongoni mwa maeneo muhimu katika kuleta kura za kumpeleka mgombea huyo kwenye ikulu ya Marekani.

Lengo la ziara ya Harris na mgombea Gavana Walz ni kuwahamasisha wapiga kura vijana, tabaka la wafanyakazi na wote waliochangia katika ushindi wa Rais Joe Biden katika uchaguzi wa mwaka 2020.