1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harris amteuwa Gavana wa Minnesota Tim kuwa mgombea mwenza

6 Agosti 2024

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amemchagua Gavana Tim Walz kuwa mgombea mwenza wake. Hii ni baada ya mchakato mkali wa uteuzi ulioanza chini ya wiki mbili zilizopita.

https://p.dw.com/p/4jBG8
Marekani | uchaguzi 2024 | Kamala Harris na Tim Walz
Mgombea urais Marekani wa chama cha Demokratic Kamala Harris akiwa na mgombea mwenza Tim Walz.Picha: Stephen Maturen/Getty Images

Harris ametangaza uamuzi huo kupitia ujumbe wa video kabla ya viongozi hao wawili kuelekea katika mkutano wa hadhara jimboni Philadelphia.

Katika kumchagua Walz, gavana wa Minnesota mwenye umri wa miaka 60, anamtegemea veterani huyo wa kijeshi aliyesaidia katika utekelezaji wa ajenda kabambe ya chama cha Democratic katika jimbo lake, ikiwemo ulinzi mkubwa wa haki za utoaji mimba na misaada mikubwa kwa familia zenye uhitaji. 

Soma pia:Kambi ya kampeni ya Kamala kuelekea uchaguzi ujao

Gavana Walz anajiunga na Harris ambaye sasa ni rasmi, ndiye mgombea wa urais kwa tiketi cha chama cha Democratic, katika mojawapo ya vipindi vigumu zaidi katika siasa za karibuni za Marekani na kuweka mazingira ya kuwepo na kampeni kali na zisizotabirika za uchaguzi wa rais.

Warepublican wameungana na mgombea wao rais wa zamani Donald Trump hasa baada ya jaribio la mauaji dhidi yake mwezi Julai.