SiasaAsia
ASEAN yatoa wito wa kuwepo suluhisho la amani kwa mizozo
27 Julai 2024Matangazo
Viongozi hao wamezitaka pande zote kukomesha vita na kufuata mpango wa amani ulioafikiwa. Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa siku mbili baada ya mkutano wao huko Laos, viongozi hao walipongeza hatua za kupunguza hali ya mivutano katika Bahari ya Kusini mwa China.
Soma pia: Mawaziri wa ASEAN wakutana huko Laos
Mawaziri hao wa ASEAN wameelezea majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini kuwa ni matukio ya kutisha huku wakihimiza kuwepo kwa suluhisho la amani katika migogoro ya Ukraine na Gaza, wakielezea wasiwasi wao juu ya hali mbaya ya kibinadamu katika maeneo hayo.