1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu zaidi waliokumbwa na mafuriko Ujerumani wahamishwa

3 Juni 2024

Vikosi vya uokozi nchini Ujerumani vimeendelea kuwahamisha watu walioko kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko kusini mwa Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4gb0i
Mafuriko Ujerumani | Bavaria
Kansela Olaf Scholz na viongozi wa jimbo la Bavaria wakitembelea maeneo yaliyoathiriwa kwa mafuriko.Picha: Oliver Pieper/DW

Hayo yanajiri wakati Kansela Olaf Scholz akitahadharisha kwa kusema hili ni kama onyo kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanazidi kuongezeka.

Scholz ambaye ameyatembelea maeneo yaliyoathiriwa aidha amevishukuru vikosi hivyo na kusema wamejaribu sana kuzuia majanga makubwa zaidi na kuokoa maisha.

"Hii ni mara ya nne mwaka huu nakwenda kwenye eneo kunakofanyika operesheni kujionea kinachoendelea huko. Na hiyo pia ni dalili kwamba kuna kitu kinaendelea. Kwa hivyo hatupaswi kupuuza kazi ya kuzuia athari za mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababishwa na mwanadamu" amesema kiongozi huyo.

Maelfu ya watu kwenye jimbo la Bavaria na Baden Wuerttenberg walilazimika kuondoka kwenye makazi yao tangu mvua kubwa ziliponyesha siku ya Ijumaa na kusababisha mafuriko makubwa.

Waziri mkuu wa  Bavaria Markus Soeder, aliyeandamana na Scholz katika ziara hii kwa upande wake alitahadharisha juu ya majanga zanazoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa akisema hakuna "bima kamili" dhidi ya mabadiliko hayo.