1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Joto la siasa lazidi Tanzania

9 Julai 2020

Joto la kisiasa katika mikoa ya kanda ya kaskazini mwa Tanzania linaendelea kupamba moto wakati ambapo wanasiasa wanaotaka kuwania nafasi za ubunge katika majimbo ya uchaguzi wakiongezeka.

https://p.dw.com/p/3f3uF
Tansania Wahlen CHADEMA Partei
Picha: DW/V. Natalis

Katika jimbo la Arusha mjini mkoani Arusha eneo ambalo ni ngome ya chama kikuu cha upinzani nchini humo CHADEMA, idadi ya waliotia nia kugombea ubunge katika jimbo hilo kupitia chama hicho imefikia watu watatu huku wanachama wengine wakikihama chama hicho na kujiunga na CCM.

Godbless Lema aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arush mjini kupitia tiketi ya Chadema, ametangaza tena kuwa atagombea ubunge wa jimbo hilo.

Katika ofisi za Chadema kanda ya kaskazini zilizopo Arusha Lema amewakilishwa na mke wake bi Neema Godbless Lema wakati wa kuchukua fomu hiyo, baada ya kuelezwa kuwa Lema amepata udhuru wakati yupo njiani kuelekea katika ofisi za Chadema Kanda ya kaskazini.

Wanasiasa wa Chadema wahama chama chao na kujiunga na CCM

Wakati wa kuchukua fomu hiyo kwa niaba ya mume wake bi Neema amesema.

Katika hatua nyingine wanasiasa wa chama cha chadema wameendelea kukihama chama hicho na kujiunga na CCM kwa madai ya kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

Katika hali isiyotarajiwa,aliyekuwa mbunge wa Arumeru mashariki kupitia Chadema Joshua Nassari jana ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM kwa madai hay ohayo ya kuunga mkono juhudi za Rais jambo ambalo yeye mwenye alilikanusha wakati akiwa mbunge wa Chadema.

Hali hiyo inaacha maswali kwa watu wengi kuwa ni kipi wakiamini kutoka kwa wanasiasa hasa kipindi hichi nchi hiyo inapoelekea katika uchaguzi mkuu mwezi October mwaka huu. Hata hivyo mchuano ni mkali zaidi katika mikoa ya kanda ya kaskazini yenye majimbo ya uchaguzi yapatayo 35.