1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya hekta 17,000 za nyika zateketea kwa mioto Australia

27 Januari 2024

Zaidi ya hekta 17,000 za nyika zimeteketezwa kwa mioto nchini Colombia tangu mwezi Novemba, wakati nchi hiyo ikikabiliwa na joto kali zaidi la mwezi Januari ambalo halijashuhudiwa kwa miongo kadhaa.

https://p.dw.com/p/4bk5x
Australien | Moto wa msitu uliosababishwa na radi
Moto na moshi vikiwa vimetanda baada ya radi kupiga na kusababisha kuibuka kwa mioto katika jimbo la Narrabri nchini australia, Disemba 09, 2023Picha: Jen Osborne/Anadolu/picture alliance

Waziri wa Mazingira wa Colombia Susana Muhamad amesema taifa hilo  limerekodi zaidi ya mioto 340 katika kipindi hicho iliyochochewa na ukame wa muda mrefu, joto kali na hali ya hewa ya El Nino na kuongeza kuwa mioto 26 bado inaendelea kuwaka.

Colombia imekuwa ikikabiliana na mioto kadhaa karibu na mji mkuu tangu siku ya Jumatatu na kwenye baadhi ya milima inayozunguka Bogota.

Mamlaka imewashauri wakazi wanaoishi karibu na maeneo yaliyoteketezwa kutotoka nje kutokana na hali mbaya ya hewa.