1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Ukraine ladunguwa droni 13

5 Aprili 2024

Jeshi la anga la Ukraine limedai kudungua ndege 13 zisizo na rubani kufuatia mashambulizi ya usiku kucha yaliyofanywa na Urusi kwenye mikoa ya kusini mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4eSLn
Ukraine | mashambulizi ya droni Urusi
Athari za mashambulizi ya droni za Urusi kwenye mji wa Kharkiv ulioko mashariki mwa Ukraine.Picha: Vitalii Hnidyi/REUTERS

Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa siku ya Ijumaa (Aprili 5) ilisema ndege zisizo na rubani aina ya Shahed ziliharibiwa juu ya anga ya mikoa ya Zaporizhzhia, Odesa na Dnipropetrovsk. 

Inaarifiwa kwamba Urusi pia ilitumia makombora ya masafa marefu katika mashambulizi hayo.

Soma zaidi: Urusi na Ukraine zaendelea kushambuliana kwa ndege za droni

Aidha maafisa wa Ukraine waliripoti mripuko katika shambulizi jengine mashariki mwa Kharkiv. 

Wizara ya ulinzi ya Urusi iliripoti kwamba imedunguwa ndege 53 za Ukraine zisizo na rubani, nyingi zikilenga eneo la kusini la Rostov.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram, Gavana Vasily Golubev wa Rostov alisema shambulizi hilo liliharibu kituo kidogo cha umeme na kuwaacha baadhi ya wakaazi bila ya huduma hiyo.