1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi na Ukraine zaendelea kushambuliana kwa ndege za droni

25 Machi 2024

Watu kadhaa wamejeruhiwa kusini mwa Ukraine, kutokana na shambulio lililofanywa na Urusi kwa kutumia ndege zisizo na rubani.

https://p.dw.com/p/4e69s
Ukraine | Kiev
Jengo lililoharibiwa vibaya nchini Ukraine kufuatia makombora yaliyorushwa na Urusi mjini KievPicha: Gleb Garanich/REUTERS

Ukraine imesema ndege hizo zilishambulia kwenye majimbo ya Odessa.

Gavana wa jimbo la Odessa Oleg Kipper, amesema miundombinu ya nishati iliharibiwa katika mashambulio hayo na kwamba ugavi wa nishati kwenye baadhi ya sehemu za jimbo hilo umekatizwa. Mashambulio mengine kwenye jimbo jingine la Ukraine la Mykolaiv. watu 11 walijeruhiwa.

Urusi yawaweka kizuizini washukiwa wa ugaidi

Wakati huo huo moto uliripuka baada ya ndege za droni za Ukraine kukishambulia kituo muhimu cha nishati cha Urusi katika jimbo la nchi hiyo la Rostov. Jimbo hilo la mpakani ni makao yanayotumiwa na jeshi la Urusi kupanga vita dhidi ya Ukraine.

Katika shambulio jingine kusini magharibi mwa Urusi vituo viwili vya nishati vilishambuliwa na ndege za droni za Ukraine. Urusi imesema imezidungua droni 11 za Ukraine katika  jimbo hilo la Rostov.