JamiiUganda
Mwanaharakati wa jamii ya LGBTQ nchini Uganda ashambuliwa
4 Januari 2024Matangazo
Kulingana na jeshi la polisi la Uganda hali ya mwanaharakati huyo wa jamii ya LGBTQ ni mbaya sana.
Video kwenye mtandao wa X inamuonyesha Kabuye akiwa amelala chini na mwenye maumivu makali, jeraha kubwa la kisu kwenye mkono wa kulia na kisu kilichonasa tumboni.
Msemaji wa polisi Patrick Onyango amesema watu walimkuta Kabuye akiwa na hali mbaya baada ya kushambuliwa.
Kabuye amedai kwamba washambuliaji hao walinuia kumuua na si kumpora na kuongeza kuwa wamekuwa wakimfuatilia kwa siku kadhaa.
Wanaharakati wa jamii hiyo nchini Uganda wamekuwa wakielezea hofu yao tangu taifa hilo lilipopitisha sheria mpya dhidi ya jamii hiyo, wakisema itaongeza mashambulizi dhidi yao.