1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yagundua handaki kubwa zaidi linalotumiwa na Hamas

18 Desemba 2023

Jeshi la Israel limesema limegundua handaki kubwa linalotumiwa na wanamgambo wa kundi la Hamas mita chache tu kutoka kwenye kivuko cha mpaka cha Erez.

https://p.dw.com/p/4aHHX
Ukanda wa Gaza |  Handaki linalotumiwa na kundi la Hamas
Wanajeshi wa Israel wakisimama mbele ya handaki linaloaminika kutumiwa na kundi la HamasPicha: Amir Cohen/REUTERS

Jeshi hilo la IDF limeongeza kuwa, handaki hilo limegunduliwa karibu mita 100 kusini mwa kituo cha ukaguzi cha Erez, ambacho ni kivuko cha mpaka kati ya Israel na Gaza.

IDF imelitaja handaki hilo kama moja ya nyenzo muhimu za kundi la Hamas ambalo hutumiwa kupitisha vifaa na bidhaa nyengine za wapiganaji wa Hamas kutoka Gaza hadi kwenye mpaka wa Israel.

Msemaji mkuu wa jeshi la Israel Rear Admiral Daniel Hagari amesema hilo ni handaki kubwa zaidi kuwahi kuliona huko Gaza na kwamba fedha na muda mwingi ulitumika kulijenga handaki hilo.

Jeshi hilo pia limeeleza kuwa, limepata silaha nyingi zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye handaki hilo, tayari kutumika kufanya mashambulizi.