Israel yatoa agizo kwa wakaazi wa Baalbek, Lebanon kuhama
3 Novemba 2024Hii ni baada ya ving'ora kuanza kulia kwenye mpaka wa Israeli kutokana na kurushwa kwa roketi kutoka Lebanon.
IDF inaendeleza mashambulizi makhsusi kusini mwa Lebanon ili kuwaangamiza wapiganaji wa Hezbollah na imedai kuzuwia makombora kadhaa yaliofyatuliwa nchini Israel, huku mengine yakianguka katika maeneo ya wazi.
Mashambulizi ya karibuni ya roketi kutoka Lebanon yalisababisha vifo saba katika eneo la Metula nchini Israel.
IDF imedai pia kugundua idadi kubwa ya silaha kusini mwa Lebanon na kukabiliana na kile ilichokiita magaidi. Tangu Septemba 23, mzozo huo umesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,900 nchini Lebanon na vifo vya wanajeshi 38 wa Israeli.
Soma pia:Khamenei aapa kuishambulia tena Israel, Marekani yaonya
Mzozo uliongezeka baada ya Hezbollah kuanza kurusha makombora mnamo Oktoba 8 katika hatua ya kuiunga mkono Hamas, kufuatia shambulio lake dhidi ya Israeli Oktoba 7 2023, ambalo lilisababisha vifo vya watu 1,206 nchini Israeli.
Majibu ya kijeshi ya Israeli katika Ukanda wa Gaza yamesababisha vifo vya Wapalestina 43,341, wengi wao wakiwa raia.