1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGabon

Jenerali Brice Oligui Nguema kuapishwa leo

4 Septemba 2023

Jenerali wa kijeshi aliyepewa uongozi wa nchi baada ya mapinduzi wiki iliyopita nchini Gabon anaapishwa leo kuwa rais wa mpito.

https://p.dw.com/p/4VvDf
Gabun | General Brice Oligui Nguema
Picha: AFP/Getty Images

Jenerali Brice Oligui  Nguema ambaye ni kiongozi wa jeshi maalum la ulinzi wa Jamhuri,na ambaye aliongoza maafisa wa kijeshi kufanya mapinduzi Jumatano dhidi ya serikali ya rais Ali Bongo Ondimba,anakabidhiwa rasmi uongozi wa nchi kwa muda usiojulikana.

Nchi nyingi za Magharibi zimelaani mapinduzi hayo ya Gabon. 

Mara kadhaa kiongozi huyo wa kijeshi ameahidi kuandaa uchaguzi huru,wa haki na kuaminika bila ya kutaja lini hatua hiyo itachukuliwa,ingawa ameshaweka wazi kwamba mchakato huo hauwezi kufanyika kabla kwanza kuidhinishwa  katiba mpya kupitia kura ya maoni.  

Soma pia:Kiongozi wa kijeshi nchini Gabon asema hatoharakisha uchaguzi

Nchi nyingine hazimtambui jenerali huyo kama kiongozi halali wa Gabon na anakabiliwa na shinikizo la kuweka wazi mipango yake ya kurudisha utawala wa kiraia.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW