SiasaGabon
Gabon yafungua mipaka siku tatu baada ya mapinduzi
2 Septemba 2023Matangazo
Msemaji wa jeshi la nchi hiyo amearifu kupitia televisheni ya taifa kwamba, mipaka ya bahari, nchi kavu na anga ya Gabon imefunguliwa kwa sababu viongozi wa kijeshi wanataka kuheshimu utawala wa sheria, mahusiano mema na nchi jirani pamoja na mataifa yote duniani.
Kulingana na msemaji huyo wa jeshi, hatua hiyo pia imechukuliwa ili kuonesha wajibu wa nchi hiyo kwa Jumuiya ya Kimataifa.
Mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini humo Jumatano wiki hii chini ya Jenerali Oligui Nguema ni ya nane kwenye mataifa ya Magharibi na Kati mwa Afrika ndani ya miaka mitatu.
Hali hiyo imezua hofu kuhusu majeshi kufanya mapinduzi kote katika ukanda huo na kufuta maendeleo ya kidemokrasia yaliyofikiwa ndani ya miongo miwili iliyopita.