Je ni kweli kwamba "Magari makubwa = Faida kubwa?"
Sio muda mrefu uliopita, iliaminika kwamba magari makubwa ya kifahari hutengeneza faida kubwa kwa wazalishaji. Lakini kulingana na utafiti mpya, hili si ukweli tena, ingawa kwa baadhi ya chapa bado lina ukweli.
Mambo mazuri kwa Ferarri.
Katika nusu ya mwaka wa 2018, kila Ferrari ilitengeneza takriban Dola 80,000 za faida ya uendeshaji, ambayo hailinganishwi na mzalishaji mwingine yoyote wa magari. Hii ni kulingana na utafiti wa mpya uliofanywa na mtaalamu wa magari wa Ujerumani, Ferdinand Dudenhöffer.
Porsche: Kampuni inayofuatia.
Porsche ni mzalishaji wa magari ya kifahari anayepata faida kubwa nchini Ujerumani, ambaye anajiingizia Euro 17,000 ya mapato ya kabla ya kodi kwa kila gari linalouzwa, hivyo kuwaacha mbali kabisa wapinzani wake wa ndani.
Chapa za magari za Ujerumani zinafanya vizuri.
Wakati Porsche ikiwa imejiimarisha kileleni, washindani wake wa ndani, BMW, Mercedes na Audi wenyewe hujipatia wastani wa Euro 3,000 kwa kila gari, kwa kuangazia kigezo cha faida ya uendeshaji.
Bado ina faida..
Magari kutoka kampuni kubwa ya magari ya Uingereza, Jaguar Landrover, huingiza Euro 800 kwa kila gari. Magari makubwa, lakini hayana faida kubwa sana, lakini hali inaweza kuwa mbaya zaidi....
Inagharimu, sio tu wanunuzi.
...kama unavyoona kupitia mfano wa magari ya Tesla, chini ya mwanzilishi mwenza aliyetambulika sana Elon Musk. Tesla, ambalo ni moja ya magari ya kifahari bado haijaweza kutengeza faida. Na badala yake, inaigharimu kampuni takriban Euro 11,000.
Bentley kinazidi kurudi nyuma.
Kulingana na utafiti huo wa Dudenhöffer, hali ni mbaya zaidi kwa magari ya kifahari ya Bentley. Utafiti unasema magari hayo yanayozalishwa na kiwanda chenye makao yake eneo la Cheshire, Uingereza hivi sasa hakifaidiki chochote, na badala yake kimeendelea kupata hasara, kwa kiwango cha Euro 17,000 kwa kila gari lililouzwa.