1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jamii asilia, Brazil zashinikiza ardhi yao kutambuliwa

26 Aprili 2024

Maelfu ya watu wa jamii za asili nchini Brazil wameandamana jana Alhamisi katika mji mkuu Brasilia wakiitaka serikali kutambua rasmi ardhi waliyoishi kwa miongo mingi.

https://p.dw.com/p/4fCSx
Brasilia | Waandamana kutaka ardhi yao kulindwa
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva akizungumza na Waziri wa Jamii za Asili Sonia Guajajara wakiwa kwenye mkutano na viongozi wa jamii hizo Picha: Adriano Machado/REUTERS

Jamii hiyo ya asili pia imeitaka serikali kulinda maeneo yao dhidi ya shughuli za kihalifu kama uchimbaji haramu wa madini.

Waandamanaji hao waliekea eneo kuliko na jengo la Bunge, Mahakama ya Juu na Makazi ya Rais mjini Brasilia.

Kundi la viongozi wa jamii hizo waliingia na kuzungumza na Rais Luiz Inacio Lula da Silva kwenye makazi ya rais, huku waliobaki nje wakipaza sauti wakisema haki zao, si suala la mjadala.

Karibu asilimia 13 ya Brazil ni maeneo ya jamii asilia na mengi ya maeneo hayo yako katika msitu wa Amazon.