1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jaji Nigeria awapa dhamana watu 10 walioshtakiwa kwa uhaini

11 Septemba 2024

Jaji mmoja katika mahakama ya Nigeria, amewaachilia kwa dhamana watu 10 waliokuwa wameshtakiwa kwa kosa la uhaini na kula njama ya kuchochea uasi wa kijeshi.

https://p.dw.com/p/4kWHI
Jeshi la Nigeria
Jeshi la NigeriaPicha: Sunday Alamba/AP Photo/picture alliance

Jaji mmoja katika mahakama ya Nigeria, amewaachilia kwa dhamana watu 10 waliokuwa wameshtakiwa kwa kosa la uhainina kula njama ya kuchochea uasi wa kijeshi kufuatia maandamano yaliyozuka mwezi uliopita nchini humo, ya kupinga ongezeko la gharama za maisha.Jeshi la Nigeria laonya dhidi ya ghasia za mtindo wa Kenya

Jaji Emeka Nwite amewapa dhamana wanaume tisa na mwanamke mmoja kwa kutumia mamlaka yake baada ya kujiridhisha kutokana na tahmini aliyoifanya. Watuhumiwa hao wote walikanusha mashtaka yanayowakabili. Wanigeria waliandamana kwa siku 10 mwezi uliopita kulalamikia mfumuko wa bei uliosababisha hali ngumu ya maisha kwa wakaazi wengi. Maandamano hao yalishuhudia maelfu ya watu wakiingia mitaani, lakini yalidhibitiwa na vikosi vya usalama vilivyotawanywa katika miji ya nchi hiyo na takriban watu 13 waliuwawa.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW