1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ndege ya Lbya yaenda Italia

30 Septemba 2023

Mamlaka nchini Libya zimetangaza kurejesha safari za ndege za kibiashara kati yake na Italia ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika kipindi cha takriban muongo mmoja.

https://p.dw.com/p/4X0Tf
Abdul Hamid Mohammed Dbeibah
Picha: Mohammed El Shaikhy/AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa mamlaka ya viwanja vya ndege ya Italia, ndege chapa MT522, ya shirika la ndege la Libya, Medsky iliondoka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mitiga huko Tripoli kuelekea uwanja wa ndege wa Leonardo da Vinci wa mjini Roma.Serikali ya Waziri Mkuu Abdul-Hamid Dbeibah mjini Tripoli imepongeza hatua hiyo, na picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zimeonesha abiria waliokuwa wakipanda ndege hiyo na viongozi wakisherehekea.Italia na mataifa mengine ya magharibi yalizua safari za ndege za Libya baada ya taifa hilo kukumbwa na vita, vilivyoungwa mkono na Jumuiya ya Kujihami ya NATO na kusababisha kupinduliwa kwa aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Moummar Gadhafi mnamo mwaka 2011.