UhamiajiItaly
Italia yapitisha kanuni mpya kuwakabili wahamiaji
19 Septemba 2023Matangazo
Baraza la Mawaziri la nchi hiyo limepitisha uamuzi huo jana jioni ikiwa ni hatua ya hivi karibuni kabisa ya kukabiliana na wimbi la wahamiaji wanaongia Italia, wengi kutoka barani Afrika.
Waziri Mkuu anayegemea siasa za mrengo mkali wa kulia, Giorgio Meloni, amesema uamuzi uliopitishwa utaruhusu wahamiaji kuwekwa kizuizini kwa muda wa kati ya siku 135 na usiozidi miezi 18 kabla ya kurejeshwa walikotoka.
Amesema serikali yake inataka kutuma ujumbe kote barani Afrika kwamba Italia itawachukulia hatua wote watakaovunja sheria kwa kujaribu kuingia nchini humo kwa njia za magendo.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya idadi kubwa ya wahamiajikuingia kwenye kisiwa cha Lampedusa ndani ya wiki chache zilizopita wakitokea kaskazini mwa Afrika.