1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia makao makuu ya Hezbollah, Beirut

28 Septemba 2024

Israel imesema imefanya mashambulizi kwenye makao makuu ya kundi la Hezbollah mjini Beirut na kwamba mkuu wa kundi hilo Hassan Nasrallah ndiye aliyekuwa akilengwa.

https://p.dw.com/p/4lBag
Lebanon | Moshi ukifuka mjini Beirut kufuatia mashambulizi ya Israel
Moshi ukifuka katika mhi mkuu wa Lebanon- Beirut kufuatia mashambulizi ya IsraelPicha: Hassan Ammar/AP/dpa/picture alliance

Jeshi la Israel limesema pia kuwa limemuua kamanda  wa Hezbollah Muhammad Ali Ismail na naibu wake Hossein Ahmed Ismail kusini mwa Lebanon.

Makabiliano hayo yanajiri baada Waziri Mkuu wa Israel  Benjamin Netanyahu  kuihutubia hapo jana hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa na kuapa kupigana kuwalinda watu wake.

Hata hivyo kundi la Hezbollah  limetangaza kuwa kiongozi wake yuko salama na kwamba wamejibu mashambulizi kwa kurusha makombora kuelekea mji wa kaskazini mwa Israel wa Safed.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress amesema anaunga mkono mpango wa usitishwaji mapigano huko Lebanon na kuonya kuwa eneo la Mashariki ya Kati liko hatarini kutumbukia katika janga kubwa.