1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yakumbuka mauaji ya Holocaust

Thelma Mwadzaya20 Aprili 2009

Israel inaadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya Wayahudi milioni 6 yaliyotokea wakati wa vita vya pili vya dunia.Kwa mujibu wa mashirika ya kuhamasisha umma kuhusu mauaji hayo zaidi ya wahanga 230,000

https://p.dw.com/p/HaWa
Picha ya kambi moja ya Wayahudi kulikotokea mauaji ya HolocaustPicha: AP/DW
Auschwitz Holocaust Gedenktag
Kumbukumbu ya kambi ya Auschwitz iliyoko kusini mwa PolandPicha: AP

'Maadhimisho hayo yamepangwa kufanyika katika jumba la kitaifa la makumbusho kwa ajili ya mauaji ya wayahudi yaliyotokea katika vita vya pili dunia.


Rais Shimon Peres wa Israel pamoja na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo inayofanyika katika jumba la Yad Vasdhem la makumbusho.Viongozi wawili wa wakuu wa kidini nchini humo wanatazamiwa kuwasha mishumaa sita vilevile kufanya misa maalum.Ving'ora vilisikika kote nchini kwa dakika nzima huku magari yote yakisimama na watu kutulia tuli.

Deutschland Holocaust Gedenkstätte Konzentrationslager Dachau
Kambi ya mauaji ya DachauPicha: picture-alliance/ dpa

'Wakati huohuo maelfu ya watu wamemiminika katika jumba jipya la makumbusho lililofunguliwa rasmi hii leo katika eneo la Chicago nchini Marekani.Mikanda ya Rais Barack Obama wa Marekani ilifungua rasmi shughuli hiyo.Katika hotuba yake Rais Obama alisisitiza umuhimu wa kuwafahamisha watoto kuhusu ukatili dhidi ya ubinadamu.Rais Obama alisema kuwa pindi watoto watakapozuru jumba la Skokie wataweza kufahamu umuhimu wa kuheshimu ubinadamu.

Ufunguzi rasmi wa jumba hilo ulifanyika hapo jana na kuhudhuriwa pia na gavana wa Illinois Pat Quinn.


Jumba hilo lililo na ukubwa wa futi alfu 65 mraba linaripotiwa kuwa kubwa zaidi katika eneo hilo.Ushuhuda wa wahanga alfu 2 wa mauaji ya wayahudi unaripotiwa kuhifadhiwa katika jumba hilo la Skokie.Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton anatazamiwa kutoa hutuba muhimu hii leo katika jumba hilo.

Kwa upande mwengine Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amewashtumu vikali wote wanaodharau umuhimu wa siku hii kadhalika wanaoshikilia kuwa mauaji hayo hayakufanyika.

Mwaka 2007 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa liliidhinisha azimio linalosisitiza umuhimu wa kuyakumbuka mauaji hayo ya kikatili kwa minajili ya kuzuia uwezekano wa kutokea tena.











Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi