Israel yakanusha kuvujisha mkutano na waziri wa nje wa Libya
28 Agosti 2023Hata hivyo, wizara hiyo haikuweka wazi ni nani aliyevujisha habari za kikao hicho kilichotajwa kama hatua ya awali kabisa ya kidiplomasia kati ya Libya na Israel.
Inasemekana mawaziri hao walizungumzia, pamoja na masuala mengine, namna ya kuwa na mahusiano mazuri baina ya mataifa yao.
Soma zaidi: Mwanadiplomasia wa juu Libya asimamishwa kazi baada ya kukutana na mwenzake wa Israel
Israel na Libya hazina mahusiano ya kidiplomasia na kisheria ni kosa kwa afisa ama raia wowote wa Libya kuanzisha mahusiano yoyote na Israel.
Tangazo la mkutano huo liliibua maandamano katika baadhi ya miji ya Libya hatua iliyochochea Mangoush kusimamishwa kazi na Waziri Mkuu Abdulhamid Dbeibah.
Kulingana na shirika la habari la Anadolu la nchini Uturuki, Mangoush tayari ameondoka kuelekea Istanbul kufuatia mzozo huo wa kidiplomasia, ingawa bado hakujatolewa taarifa rasmi.