1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel yafanya mashambulizi mapya nchini Lebanon

27 Septemba 2024

Serikali ya Israel imetupilia mbali pendekezo la kusitisha mapigano kwa siku 21 nchini Lebanon, na kuahidi kuendelea kupambana na wanamgambo wa Hezbollah hadi watakapopata ushindi kamili.

https://p.dw.com/p/4l9GQ
Lebanon-Uharibifu wa shambulizi la Israel
Lebanon-Uharibifu wa shambulizi la IsraelPicha: Louisa Gouliamaki/REUTERS

Serikali ya Israel imetupilia mbali pendekezo la kusitisha mapigano kwa siku 21 nchini Lebanon, na kuahidi kuendelea kupambana na wanamgambo wa Hezbollah hadi watakapopata ushindi kamili.Israel yaapa kuendelea kupambana na Hezbollah hadi ushindi

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema hakujibu pendekezo linaloongozwa na mfadhili wake mkuu Marekani kwa ushirikiano na Ufaransa na kwamba amewaamuru wanajeshi wake kuendeleza mapigano kwa nguvu zote.

Usiku wa jana, Israel imefanya mashambulizi mapya na kuyalenga maeneo kadhaa ya kundi la Hezbollahkusini mwa Lebanon. Shambulio jingine katika vitongoji vya kusini mwa Beirut lilimuua mkuu wa kitengo cha droni wa Hezbollah Mohammed Srur.

Miito ya kimataifa imeendelea pia kutolewa na kuzitaka pande zote kujizuia ili kuzuia mzozo huo kutanuka zaidi.