1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel: Mashambulizi yatasitishwa tutapoitokomeza Hamas

12 Desemba 2023

Israel imeendelea na mashambulizi yake dhidi ya kundi la wanamgambo la Hamas na imesema mapigano hayo huenda yakaendelea kwa wiki kadhaa au hata miezi.

https://p.dw.com/p/4a4D7
Israel | Wanajeshi wa Israel wakiwa na magari ya kijeshi wakiingia katika Ukanda wa Gaza
Magari ya kijeshi na askari wa Israel wakiiingia katika eneo la Ukanda wa Gaza kuongeza nguvu ya kijeshiPicha: Amir Cohen/REUTERS

Wakati Baraza la Umoja wa Mataifa likitarajiwa kupiga kura baadae hii leo, Israel na Marekani zimeendelea kushinikizwa kuridhia kusitisha mapigano katikaUkanda wa Gaza.

Wiki iliyopita Marekani ilizuwia azimio la Baraza la Usalama lililokuwa na lengo la kuhimiza usitishwaji huo wa mapigano Gaza.

Rais wa taifa hilo Joe Biden ameendelea kusisitiza haki ya Israel kujilindaakisema kwamba ataendelea kujitolea kwa ajili ya usalama wa Wayahudi na Israel na haki ya kuwepo kama taifa huru.

Soma pia:Israel yakanusha kutaka kuwahamishia Misri wakaazi wa Gaza

Zaidi ya wapalestina 17,000 wameuwawa katika ukanda huo, wengi wao wakiwa wanawake na watoto hii ikiwa ni kulingana na data za wizara ya Afya inayodhibitiwa na Hamas, Kundi aambalo Israel, Marekani na nchi nyingine zimeliorodhesha kuwa la kigaidi.

Takriban asilimia 90 ya watu wa Gaza ambao ni watu milioni 2.3 wamepoteza makaazi yao huku Umoja wa Mataifa ukis