Gaza ni 'jehanamu ya dunia' - Lazzarini
11 Desemba 2023Kauli hiyo ya mkuu wa UNRWA inakuja wakati Israel ikiarifu kuwa iliyashambulia maeneo yapatayo 250 katika ukanda huo, ikidai kuwa baadhi yake ilikuwa mifumo ya njia za chini ya ardhi.
Wakati huo huo, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limepitisha azimio linalotaka msaada kibinadamu ufikishwe mara moja katika Ukanda wa Gaza.
Soma zaidi: Idadi ya waliofariki Gaza yaongezeka baada ya mapigano kuanza tena
Marekani haikulipinga azimio hilo ingawa imesema linaegemea upande mmoja.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema kuwa mgogoro wa sasa umeanika kweupe kupooza kwa Baraza la Usalama.
Huku hayo yakiarifiwa, maelefu ya watu waliandamana jana Jumapili nchini Ujerumani na Ubelgiji, wakilaani chuki dhidi ya Wayahudi na ubaguzi wa rangi.