1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yawanyonga watuhumiwa wanne waliohusishwa na Mossad

29 Januari 2024

Iran imewanyonga watu wanne waliohukumiwa adhabu ya kifo baada ya kuhusishwa na operesheni ya ujasusi ya Israel.

https://p.dw.com/p/4bmjb
Polisi wa Iran wanajitayarisha kuwanyonga hadharani wafungwa mjini Tehran
Polisi wa Iran wanajitayarisha kuwanyonga hadharani wafungwa mjini Tehran Picha: Abedin Taherkenareh/EPA/picture-alliance/dpa

Hukumu hiyo imetekelezwa leo Jumatatu baada ya kesi yao ya rufaa kukataliwa na mahakama ya juu ya Iran.

Watuhumiwa hao walidaiwa kuingia kwa njia zisizo halali katika ardhi ya Iran kutoka jimbo la Kurdistan nchini Iraq kwa lengo la kufanya mashambulizi ya mabomu katika kiwanda cha Isfahan cha utengenezaji vifaa vya wizara ya ulinzi ya Iran.

Inadaiwa walipanga kutekeleza mashambulio hao majira ya joto mnamo mwaka 2022 kwa niaba ya shirika la ujasusi la Israel, Mossad, lakini majasusi wa Iran wakazima jaribio hilo.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW