Iraq yalaani mashambulizi ya Marekani
24 Januari 2024Matangazo
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin, alisema vikosi vya nchi yake vilifanya mashambulizi ambayo ni ya lazima dhidi ya vituo vitatu vinavyotumiwa na wanamgambo wa Kitaeb Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran na makundi mengine yenye uhusiano na Iran yaliyo nchini Iraq.
Lakini msemaji wa Waziri Mkuu wa Iraq alisema kitendo hicho hakikubaliki, kinakiuka hadhi ya mipaka na uhuru wa taifa hilo na kinadhoofisha ushirikiano wa miaka mingi, na wakati huo huo "kinachangia kuongezeka kwa migogoro" kwenye kanda nzima ya Mashariki ya Kati.