Iran kuomboleza kwa siku tatu baada ya mauaji ya Haniyeh
31 Julai 2024Matangazo
Kundi hilo la Hamas, limesema Haniyeh atazikwa siku ya Ijumaa nchini Qatar baada ya kufanywa kwa sala ya mazishi siku ya Ijumaa.
Wakati huo huo, Iran imesema kwamba Marekani ni ya kulaumiwa katika mauaji ya Haniyeh kwasababu ya kuiunga mkono Israel.
Kwa upande wake, Umoja wa Ulaya umetoa wito wa kujizuia kwa pande husika na kuonya kuwa hakuna taifa litakalonufaika kutokana na mzozo mkubwa zaidi wa kikanda.
Kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh auwawa Iran
Hamas imesema kiongozi wake aliuawa katika shambulizi la Israel mjini Tehran wakati Haniyeh alipokuwa katika ziara mjini Tehran kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa Iran Masoud Pezeshkian.
Hata hivyo Israel bado haijazungumzia tukio hilo.
Iran na Hamas zimetangaza kulipiza kisasi.