Iran yasema Haniyeh aliuliwa kwa roketi ya masafa mafupi
3 Agosti 2024Televisheni ya taifa nchini Iran imeripoti kuwa jeshi la Walinzi wa Mapinduzi la nchi hiyo limebaini kuwa kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh aliuawa kwa kombora la masafa mafupi huku likiishutumu Marekani kwa kuiunga mkono Israel inayoshutumiwa kwa shambulio hilo.
Taarifa ya televisheni hiyo imesema roketi yenye uzito wa kilo saba ilitumika kulenga makazi ya kiongozi huyo wa Hamas katika mji mkuu Tehran siku ya Jumatano.
Taarifa hiyo inadai kuwa tukio hilo liliratibiwa na Israel na kuungwa mkono na Marekani.
Mauaji hayo kiongozi huyo wa kundi la Hamas yamezua hofu katika ukanda wa mashariki ya kati huku Iran ikisema kuwa italipiza kisasi kwa tukio hilo na Israel pia ikijibu mapigo kwamba iko tayari kwa lolote ikiwa Iran itaanzisha mashambulizi ya kulipiza kisasi.