SiasaIran
Iran yarusha setilaiti kama sehemu ya mpango wake wa nyuklia
20 Januari 2024Matangazo
Tangazo hilo, lililotolewa kupitia runinga ya taifa, limeeleza kuwa urushaji huo wa setilaiti ni sehemu ya mpango wake wa anga wa jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Kiislamu wa Iran.
Awali, Marekani iliwahi kusema kuwa urushaji wa satelaiti ya Iran unakwenda kinyume na azimio la Baraza la Usalama na kuitaka nchi hiyo kutojihusisha na shughuli zozote za kurutubisha madini ya Uranium na hivyo kuimarisha uwezo wake wa silaha za nyuklia.
Vikwazo vya Umoja wa Mataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran vilikamilika mwezi Oktoba mwaka uliopita.