1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yamkosoa Zelensky kwa kueneza propaganda dhidi yake

27 Mei 2023

Iran hii leo imemtuhumu rais wa Ukraine Volodymyr Zekenskiy kwa kueneza propaganda za kulipinga taifa hilo baada ya kuiomba kuacha kuipeekea Urusi droni.

https://p.dw.com/p/4Rt9w
Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Naser Kanaani anasema rais wa Ukraine analenga zaidi kuomba misaada na si kuituhumu Iran kwa madai ya uongo.
Iran imekuwa ikishutumiwa kwa kuipatia Urusi ndege zisizotumia rubani ambazo zimekuwa zikitumika katika mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine.Picha: jamaran

Iran aidha imesema matamshi hayakuwa lolote, wala chochote bali yalilenga kuhamasisha misaada zaidi ya silaha na fedha.    

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Nasser Kanaani amesema katika taarifa kwamba madai hayo juu ya dronizake kwenda Urusi ni ya uongo na Zelenskiy amekuwa akiyatoa mara kwa mara kwa nia ya  kuvutia msaada zaidi kutoka kwa mataifa ya magharibi.

Katika hotuba ya video aliyoitoa siku ya Jumatano Zelenskiy aliiomba Iran kuacha kujitumbukiza kwenye "upande wa giza wa kihistoria" kwa kuupatia Urusi ndege hizo zisizotumia rubani.

Iran, hapo kabla ilikana kuipatia Urusi ndege zisizo na rubani aina ya Shahed, lakini baadae ilikiri kuipatia kwa idadi ndogo kabla ya kuanza kwa mzozo kati ya Urusi na Ukraine.