1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIran

Iran yamzika jenerali aliyeuawa katika shambulio la Israel

Hawa Bihoga
28 Desemba 2023

Iran imemzika leo jenerali wake wa ngazi ya juu katika kikosi cha ulinzi wa mapinduzi aliyeuawa na kinachodaiwa kuwa shambulio la anga la Israel nchini Syria.

https://p.dw.com/p/4affY
Kiongozi wa juu kabisa nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei akitoa pole mbele ya jeneza la jenerali Seyed Razi Mousavi
Kiongozi wa juu kabisa nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei akitoa pole mbele ya jeneza la jenerali Seyed Razi Mousavi Picha: Office of the Iranian Supreme Leader via AP/picture alliance

Mamia ya waombolezaji walilisindikiza jenela la kamanda huyo Jenerali Razi Moussavi kutoka uwanja mkuu wa Tehran hadi kwenye makaburi yalioko kaskazini mwa mji huo mkuu wa Iran ambako amezikwa.

Mkuu wa kikosi cha walinzi wa mapinduzi Jenerali Hossein Salamamemsifu Moussavi na kuapa kwamba kifo chake kitalipiwa kisasi.

Salami amemuelezea Moussavi kama swahiba wa karibu wa Jenerali Qassim Soleiman, mkuu wa kikosi cha Qudsi alieuawa katika shambulio la droni la Marekani Janauri 2020.

Amesema Iran italipiza kifo cha Soleiman na kwamba mashambulizi ya Hamas kusini mwa Israel, yaliosababisha vita vya Gaza, yalikuwa hatua huru zisizohusiana na kisasi hicho.

Israel inaichukulia Iran kuwa kitisho kikubwa zaidi dhidi yake kutokana na mpango wa nyuklia wa Tehran, na uungwaji wake mkono kwa makundi kama Hamas, Hezbollah la Lebanon na waasi wa Kihouthi nchini Yemen.