1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSaudi Arabia

Iran na Saudi Arabia zarejesha uhusiano wa kidiplomasia

10 Machi 2023

Iran na Saudi Arabia zimekubaliana kufufua uhusiano wao wa kidiplomasia na kufungua tena balozi zao katika kipindi cha miezi miwili.

https://p.dw.com/p/4OWDv
Saudi-Arabien Kronprinz des Königreich Mohammed bin Salman
Picha: IMAGO/Le Pictorium

Hayo yameelezwa leo na vyombo vya habari vya nchi zote hizo mbili. Mawaziri wa mambo ya nje watakutana kwanza kuandaa mipango ya kubadilishana mabalozi na kujadili njia za kuiamrisha uhusiano. Makubaliano hayo yamefikiwa kutokana na mazungumzo yaliyofanyika China tangu siku ya Jumatatu.

Uhusiano kati ya Saudi Arabia na Iran  ulidhoofika kufuatia shambulizi lililofanywa na wapiganaji wenye itikadi kali za Kiislamu katika ubalozi wa Saudia mjini Tehran, mwaka 2016.

Oman imepongeza hatua hiyo iliyofikiwa kati ya Saudi Arabia, Iran na China. Nchi hizo tatu pia imeishukuru Oman kwa kuandaa mazungumzo yaliyofanyika awali.