Biashara
Iran na Pakistan kuimarisha ushirikiano wa kibiashara
22 Aprili 2024Matangazo
Rais wa Iran Ebrahim Raisi pamoja na Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif wameapa kuimarisa uhusiano wa kibiashara baina ya mataifa hayo jirani ya hadi dola bilioni 10 kwa mwaka, wakati Raisi akianza ziara ya siku tatu katika mji mkuu wa Pakistan, Islamabad.
Kulingana na ofisi ya Shariff, pande hizo mbili zimekubaliana kuimarisha uhusiano huo wa kibiashara katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Wamekubaliana pia kushirikiana katika kuendeleza kwa pamoja mbinu za kukabiliana na changamoto za pamoja ikiwemo kitisho cha ugaidi, imeongeza taarifa hiyo.
Raisi aliyeongozana na ujumbe unaojumuisha Waziri wa Mambo ya Nje na mawaziri wengine atazuru pia mji wa Lahore, mashariki mwa taifa hilo na mji wa bandari wa Karachi, kusini mwa Pakistan.