1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Iran, Iraq zakubaliana kupambana na 'magaidi' Kurdistan

28 Agosti 2023

Iran na Iraq zimefikia makubaliano ya kuyang'anya silaha na kuyahamisha yale zinazoyaita 'makundi ya kigaidi' katika jimbo la Kurdistan lililo kaskazini mwa Iraq kuanzia mwezi wa Septemba.

https://p.dw.com/p/4Vduc

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran, Nasser Kanaani, amesema katika taarifa ya kila wiki kwamba chini ya makubaliano hayo, Iraq imeahidi kuwanyang'anya silaha waasi wanaotaka kujitenga na makundi ya kigaidi yaliyopo kwenye eneo hilo, kufunga kambi na kuwahamisha kabla ya Septemba 19.

Soma zaidi: Pentagon yaahidi kuendelea kuisaidia Iraq kupambana na IS

Hata hivyo hakusema watahamishiwa eneo gani na Iraq haijasema chochote juu ya makubaliano hayo.

Iran kwa muda mrefu imelishutumu jimbo hilo la Kurdistan kwa kuwahifadhi magaidi waliohusiaka na mashambulizi dhidi yake.