Iran: FIFA iipige marufuku Israel kufuatia mapigano Gaza
10 Februari 2024Katika taarifa iliyowekwa katika tovuti ya shirikisho la Iran, Jamhuri hiyo ya kiislamu iliiomba FIFA kulipiga marufuku shirikisho la Israel kushiriki shughuli zote za kandanda, na kuitaka pia FIFA na wanachama wake kuja na mikakati ya kuizuwia Israel kuendelea na uhalifu wake, na kutoa pia msaada wa chakula, maji na dawa kwa wapalestina.
Mapigano ya Gaza yalianza Oktoba saba, baada ya wanamgambo wa Hamas kushambulia Kusini mwa Israel na kusababisha mauaji ya waisrael 1,160.
UN yahofia usalama wa raia walioko Rafah
Israel nayo ikajibu kwa mashambulizi ya angani na ardhini ambayo hadi sasa yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 27,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Hayo ikiwa ni kwa mujibu wa wizara ya afya ya Gaza inayodhibitiwa na Hamas. Israel imeapa kulitokomeza kabisa kundi hilo.