IOM yataka dola bilioni 7.9 kusaidia wahamiaji
22 Januari 2024Matangazo
Ombi hili linatolewa wakati changamoto kama za mabadiliko ya tabianchi, mizozo na hali mbaya za kiuchumi na fursa vikisababisha mamilioni ya watu kukimbia makazi yao.
Ombi hili la mwaka linalifanya shirika hilo sasa kusaka zaidi ufadhili kwa ushirikiano na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa na makundi ya kibinaadamu, katika wakati ambapo wafadhili wengi wakubwa wakikabiliwa na changamto za kibajeti ama kupunguza matumizi ya misaada.
Lakini IOM yenyewe imesema wanatumaini ufadhili mkubwa utatoka kwa watu na sekta binafsi pamoja na serikali
Ombi hili ni sehemu ya mpango mkakati wa miaka mitano chini ya mkurugenzi mpya wa IOM Amy Pope na utawanufaisha watu milioni 140, wahamiaji na jamii zinazowapokea.