1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

India yaiombea Afrika uanachama wa kudumu, G20

18 Juni 2023

Waziri mkuu wa India Narendra Modi amewaandikia barua viongozi wa Kundi la G20 akipendekeza Umoja wa Afrika kupewa uanachama kamili wa kudumu wa kundi la kidiplomasia katika mkutano ujao wa kilele nchini India.

https://p.dw.com/p/4SjYm
Indien | G20
Picha: Aamir Ansari/DW

Pendekezo la waziri mkuu Narendra Modi linaashiria namna India ilivyoamua kujitolea katika kuimarisha uwakilishi wa Afrika na kushirikisha katika kuunda mahusiano ya kimataifa, chanzo kimoja kimearifu.

Kundi la G20 ni jukwaa llinalojumuisha serikali za nchi zilizoendelea na zinazoendelea kiuchumi duniani, linalotengeneza karibu asilimia 85 ya pato la ndani la ulimwengu na  zaidi ya asilimia 75 ya biashara ya kimataifa.

Kundi hili aidha linakaliwa na karibu theluthi mbili ya idadi ya watu duniani.