1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

India yaanza kuhesabu kura baada ya uchaguzi wa siki sita

4 Juni 2024

India imeanza zoezi la kuhesabu kura baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika kwa wiki sita na ambao ulikuwa kipimo cha uimara wa muongo mmoja wa Waziri Mkuu Narendra Modi anayetarajiwa kujishindia muhula wa tatu madarakani.

https://p.dw.com/p/4gdo2
India | Maafisa wa uchaguzi wakihesabu kura
Maafisa wa uchaguzi India wakihesabu kura baada ya zoezi la upigaji kura lililodumu kwa wiki sita kukamilika.Picha: Manish Swarup/AP/picture alliance

Matokeo ya awali katika uchaguzi huu ambao takriban watu milioni 970 walikuwa na haki ya kupiga kura, yameonyesha kuwa chama tawala cha Bharatiya Janata BJP cha Waziri mkuu Modi kinaongoza lakini hakikupata viti vingi bungeni kama ilivyotarajiwa. 

Soma pia:Uchaguzi wa India waingia awamu ya tano katikati mwa joto kali

Chama cha BJP ni sehemu ya muungano wa kisiasa wa vyama vya kihafidhina nchini India wa National Democratic Alliance ambao kulingana na matokeo ya awali unaongoza katika maeneo 283.

Jumla ya viti 272 vinahitajika kwa chama kuwa na wingi bungeni.