1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBrazil

Idadi ya waliofariki katika mafuriko Brazil yafikia 56

Saleh Mwanamilongo
4 Mei 2024

Shirika la Ulinzi wa raia la Brazil limesema kuongezeka kwa viwango vya maji katika jimbo la Rio Grande do Sul kulikuwa kukiyafurisha mabwawa na kutishia jiji kuu la Porto Alegre.

https://p.dw.com/p/4fVlU
Mafuriko yasababisha maafa makubwa Brazil
Mafuriko yasababisha maafa makubwa BrazilPicha: GUSTAVO GHISLENI/AFP/Getty Images

Idadi ya vifo kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na dhoruba kali kusini mwa Brazili imepanda hadi watu 56.

Shirika la Ulinzi wa raia la Brazil limesema kuongezeka kwa viwango vya maji katika jimbo la Rio Grande do Sul kulikuwa kukiyafurisha mabwawa na kutishia jiji kuu la Porto Alegre.

Huku viongozi wa mji huo wakihangaika kuwahamisha watu kwenye baadhi ya vitongoji vilivyokuwa vimezama.

Zaidi ya watu 24,000 walilazimika kuyahama makaazi yao kutokana na hali hiyo ya mafuriko. Mamlaka zimesema mvua kali na mafuriko yameathiri zaidi ya manispaa 265 huko Brazil.