1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya wakimbizi kanda ya Afrika Magharibi yaongezeka

20 Septemba 2024

Idadi ya wakimbizi na watu waliolazimishwa kuhama makwao katika eneo la Afrika Magharibi na Kati imeongezeka maradufu tangu mwaka 2019 na kufikia karibu milioni 14.

https://p.dw.com/p/4ksTn
DR Kongo Goma 2024 | Wakimbizi
Watu wamekusanyika kando ya mlipuko uliotokea katika kambi ya wakimbizi nje kidogo ya Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Kamishna Mkuu wa shirika la UNHCR kanda ya Afrika Magharibi na Kati Abdouraouf Gnon-Konde amesema idadi hiyo imepanda kutoka wakimbizi milioni 6.5 mwaka 2019 hadi milioni 13.7 mwaka huu 2024.

Soma pia: Msafara wa misaada ya kibinadamu washambuliwa mashariki mwa Kongo

Abdouraouf Gnon-Konde amewambia waandishi wa Habari mjini Abidjan kuwa, kufikia mwisho wa mwaka huu, UNHCR inatarajia idadi hiyo kupanda tena hadi watu milioni 14 au hata milioni 15 kufikia mwisho wa mwaka 2025.

Idadi hiyo hata hivyo haijumuishi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako UNHCR inakadiria kuwa karibu watu milioni saba wamelazimika kuyahama makaazi yao.