MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Msafara wa misaada ya kibinadamu washambuliwa Butembo
2 Julai 2024Matangazo
Haya ni kwa mujibu wa shirika la Uingereza la Tearfund, ambalo kupitia taarifa yake, limesema wafanyakazi wawili bado hawajulikani walipo baada ya shambulizi hilo.
Msafara huo ulikuwa ukitoka katika eneo la mapigano na kuelekea kaskazini kabla ya kushambuliwa karibu na mji wa Butembo katika eneo la Lubero na vijana walioshukiwa kuwa waasi wa M23.
Aidha Shirika la msaada la Tearfund limesema magari yao yalichomwa na kuharibiwa katika shambulizi hilo huku wakitoa wito kwa pande zote kuheshimu na kulinda wafanyakazi wa misaada na kuhakikisha usalama wao wanapotekeleza majukumu yao.