JangaJapan
Idadi ya vifo yaongezeka na kufikia 161 nchini Japan
8 Januari 2024Matangazo
Kulingana na mamlaka katika mkoa wa kati wa Ishikawa, idadi ya watu ambao hawajulikani waliko imepungua hadi 103 kutoka 195.
Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.6 katika kipimo cha Richter liliikumba miji ya Toyama, Ishikawa na Niigata, yote ikiwa kwenye kisiwa kikubwa cha Honshu kilicho kwenye mwambao wa magharibi wa Bahari ya Japan . Baadaye Mamlaka ya hali ya hewa ilitoa onyo la kutokea tsunami kubwa.
Daima nchini humo, safari za ndege zimerejea kama kawaida leo Jumatatu katika uwanja wa ndege wa Tokyo wa Haneda, siku sita baada ya kutokea ajali ya ndege mbili kugongana na kusababisha vifo vya watu watano.