JamiiJapan
Kishida: Jiografia ya Noto yakwamisha uokoaji Japan
4 Januari 2024Matangazo
Waokoaji hao wana matumaini ya kuwaokoa manusura wengi kadri itakavyowezekana katika kipindi cha siku tatu muhimu za uokozi kinachokamilika leo mchana.
Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida, amesema kuna watu wengi walionasa katika majengo yaliyoanguka wanaosubiri kuokolewa na jiografia ya eneo la Noto imeifanya kazi ya uokozi na kuwatafuta manusura kuwa ngumu.
Akizungumza katika mkutano na waandishi habari waziri mkuu Kishida pia amesema watatumia uwezo wao wote kuwaokoa watu wengi kadri itakavyowezekana kufikia jioni majira ya Japan wakati saa 72 zitakapokamilika tangu kutokea kwa janga hilo.
Amesema wamefanya kila linalowezekana kutoa msaada unaohitajika na shughuli za kuyajenga upya maeneo yaliyoathiriwa.